Thursday, May 18, 2006

Unawasikiliza hawa?






Ndesanjo ametuwekea kiunganishi kwenda kwa baadhi ya watu hawa lakini sidhani kama huwa tunajaribu kuwapitia. Hawa ni washairi wa ki-reggae wanachanganya usomaji wa mashairi na midundo ya reggae katika hali fulani ambayo inapendezesha sana mashairi yao.

Kushoto kabisa anaitwa Michael Smith yeye habari zake nyingi hazijulikani sana lakini niliwahi kupata kazi yake moja kwenye shairi la 'me cyant believe it' na lingine ambalo sikumbuki jina lake. Inasemekana kutokana na msimamo wake dhidi ya chama kilichokuwa kinatawala na ukali wa maneno yake wafuasi wa chama tawala kule Jamaika walimvamia akiwa sokoni na kumponda mawe mpaka mauti yalupompata.

Hizo mbili za katikati ni Mutabaruka maarufu kwa mashairi ya ukombozi, Yeye habari zake zipo kwenye kiunganishi katika jina lake. Nakumbuka alipohojiwa kwenye muhutasari wa maisha ya Peter Tosh alisema kwamba... unapodai haki yako huhitaji kujadiliana na mdaiwa wako maana unakuwa unaipoteza haki yako..... na katika mahojiano mengine alisema ..... Afrika inasubiri waumbaji wake.... Jaribu kumfuatilia.

Picaha ya mwisho wako wawili, kushoto ni Benjamin Zephaniah, maarufu kwa mashairi na mweusi ambaye alikataa tuzo ya OBE aliyopewa na Malkia lizabeth, rudia siku Beckham alipopewa tuzo hiyo, kwa madai malkia hawajali waafrika ili anajikomba kwake. Kulia ni Linton Kwesi Johnson, aliyeshangilia upinzani dhidi ya ubaguzi wa weusi uingereza, katika shairi hilo alisikika akisema, .... kidonge cha ukandamizwaji kilitapikwa na polisi wawili walikufa..... kama ishara ya ushindi dhidi ya ubaguzi.

Wote wanne ni wazaliwa wa Jamaika .Mutabaruka yeye anaishi Jamaika, Kwesi na Benjamin Zephaniah wanaishi uingereza.

4 comments:

mzee wa mshitu said...

Mloyi
Afadhali hawa taarifa na michango yao katika jamii zimetunzwa mpaka leo mimi na wewe tunaweza kuwarejea kama wapiganiaji wa haki za weusi kwa kutumia usanii na miziki, hivi kwetu wakina Morris Nyunyusa, Makongoro, na wengineo japo hawafanani na hawa kwa mahadhi ya miziki yao kumbukumbu ziko wapi?

mwandani said...

Hawa huwa nawasikiliza nikipata muda, wananikumbusha wakati ule rege zilivyoniingia kisawasawa. Si utani hawa mabwana wamefanikiwa kiasi kikubwa kuusambaza utamaduni wao na kuwatia watu vichaa. Basi utakuta hata watu wasio waafrika, au wajamaika - wanakuwa wanaongea patwa - pindi wakikutana na hawa watu. Mpaka wajapani wana kumbi za miziki ya rege... wenyewe wanaijiita "ludi boys" (Rude Boys)

Miye hupendelea sana kutembelea maonyesho ya wapiga rege. Wakati wa kiangazi walikuwa wakijaa sana ulaya, basi haupiti mwezi bila kuwaona - haswa wale wakongwe kama Mikael Rose, Burning, Yellowman, Israel vibrations na wengineo.

La zaidi juu ya hawa mabwana - utamaduni wao wa kichwa ngumu 'resistance' bado wanauendeleza.

Ndesanjo Macha said...

Naongeza kidogo: Mutabaruka huwa havai viatu kabisa. Hata siku moja!

Christian Bwaya said...

Ndesanjo uko siriaz kuwa huyu bwana huwa havai viatu? Ha ha haaaa! Iko kazi. Sipati picha anaishije kwa maamuzi hayo.