Friday, March 23, 2007

Bado Nipo

Habari za Mwaka mpya? Mambo mengi yamejitokeza tangu kuanza kwa mwaka huu, mengine yanakubalika na pia mengine hayakubaliki wali kutegemewa, licca ya hayo yote nilipotea kwa muda mrefu kidogo bila kutoa salaam zangu za mwaka mpya, ingawa nilipita kupokea zilizotolewa na wenzangu.
Kazi bado zinaendelea, Blog zinaongezeka na wanablog pia wanaongezeka. Yule jamaa wa annony... bado anasumbua! anaweka posting zake kwangu ambazo sijui nifanyie nini lakini we acha tuu! iko siku atakomeshwa.
Kipenzi cha afrika, Mugabe, ameingiwa na kasheshe nyingine, naona inafanana na ile iliyotokea Denmark lakini haikuwa "issue" kubwa sana kama anavyofanyiwa Mugabe ingawa hakuna mtu aliyekufa kama Denmark, Tunasimama naye na udhalimu utashindwa.
Nyumbani majambazi yamerudi tena wiki hizi zilizopita, lakini "sangoma" wao hana nguvu za kuishinda jamii, wote watatulizwa.
Sikujua kama watu huwa tunakamiana kiasi hiki bila sababu ya maana na za aibu kama madeni anayolalamika Vitali Maembe kuachiwa na kaka yake, .... kuberi dukani kwa mpemba, bangi kwa pusha jeda na gongo kwa mama ..... . Bado najifikiria hili lilikuwaje lakini nimeathiriwa na jambo hili hivyo nitaliongelea nikiwa na habari za uhakika.
Mambo yanabadilika, barabara iliyoliliwa siku nyingi, kilwa, imeanza kutengenezwa tunaomba isiwe nyembamba kama ile ya shekilango, naona sasa ndugu zetu akina baa wa ntwara watapata ahueni ya usafiri ingawa bado wana mshale wa nauli za juu unawangojea wao. Tuombe mwaka huu ubadilishe hali kidogo.
Tulipata ugeni wa kimataifa, maaskofu wa kianglikana walifanya mkutano hapa Tanzania, maazimio yao kidogo yalifanana na Watanzania, labda sababu hii ni nchi takatifu hata ukija na dhamira zako chafu hutaingia nazo! Nadhani na Umoja wa Mataifa nao uje fanya mikutano yao hapa pengine nao watafikia maamuzi yenye busara.
Jumiya ya Afrika Mashariki inatangazwa na viongozi lakini kila wakienda wananchi wanaikataa, sijui kuna nini hapa, hili sijalifuatilia vizuri maana lina mawazo yanayochanganya sana. Umoja tunauongelea siku zote, ingawa sio kama wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao formula yake anajua Mwl Nyerere peke yake naye sasa hayupo duniani, naona tuvute subira turekebishe mambo mengi kwanza kabla hatujaingia huko.
Blogu bado zinahitaji kudumishwa kwa nguvu zote.