Tuesday, June 26, 2007

Hawa wana nini kwenye vichwa vyao?

Kila mara nasikiliza rege kupata ujumbe uliopo ndani yake. Na muda huu nikiandika nimevutiwa na kazi ya Bob Andy (pichani) yeye anaanza kwenye wimbo wake wa “Fire Burning” na swali hili
“ Would I have to ask you leaders what do you have in minds?”
Naona hili swali liko kwenye wakati muafaka kwenye kipindi hiki, Napenda kumuuliza Waziri Mama wa Fedha, Anafikiria nini kwenye akili yake kupanga bajeti kama ile aliyoisoma Juzi bungeni? Isitoshe makada karibu wote wa CCM wanaiunga kwa nguvu zote sijui nao wana njama gani na sisi wafanyakazi wa nchi hii, wote wana-CCM na wapinzani.
Bajeti hii inaelekeza kupandisha bei ya bidhaa zote zijulikanazo hapa Tanzania. Sijui katika hali hii ambayo kila mtu analia hali ngumu ya maisha mwingine anataka bei zizidi kupanda, bila kutupa mkakati unaoeleweka wa kuzikabili hizo bei.
Bob Andy ameendelea kutuambia,
“You are protesting on the wrong side of the fence”
“ read the lines on your fence you will be safe for sure’
Tumepiga makelele makali sana kuonyesha kutoridhika na hiyo bajeti, lakini ikapita kwa kishindo kikali sana, na mhariri wa gazeti la chama na kongwe zaidi aliweka habari ya juu kwamba Bajeti yapita kwa kishindo!, labda ni sisi ndiyo tuliipinga tukiwa tumekaa upande mbaya ambao makelele yetu hayakusikika! Au hatukusoma ishara kwenye kuta zetu tukajiingiza kwenye haya matatizo na sasa tunajua tukiwa tumechelewa!
Nikamkumbuka Mutabaruka katika shairi lake wa “Revolutionary Words” naye alisema,
“Revolutionary words have become Entertainment, Dramatizing the suffering of people in their revolutionary words”
hiki ndiyo kilichofanyika bungeni! Makelele yote waiopiga wabunge, hasa wa CCM, yalikuwa ni maigizo ya jinsi wananchi watakavyo hangaika na kulia na mzigo waliobebeshwa na bajeti hiyo. Walipochekesha Kiasi cha kutosha wakarudia kwenye kazi yao – kudai posho zao nono. Hesabu posho za siku moja walizopewa Taifa Stars utajua wanachukua ngapi kwa siku!
Linton Kwesi Johnson naye alishatuambia kwamba,
“The JLP, cyant set wi free,
the Liberate dem cyant do it fi wi,
make dem gwaan, now wi come,
wi haffi storm like a rising sun.”

Benjamin Zephaniah yeye alikataa kupewa tuzo ya OBE (amepewa Salman Rushdie juzi juzi akazua balaa kwenye jamii ya kiislamu) na malkia wa Uingereza sababu anaendelea kuunga mkono unyonywaji na ukandamizaji unaofanyika ulimwenguni.
Bado Bob Andy aliendelea kuwakumbushia kuwa,
“ Hell a go run loose, if you don’t delivering”
huu ujumbe uwafikie wanye kazi ya kupanga na kusimamia maendeleo ya Watanzania wakae vizuri kabla jehanamu haijajifungua hapa jirani, wajue maneno aliyoingia nayo JK ikulu na wajue tupo millioni na zaidi tunaotafuta nafasi ya kuyatekeleza kwa vitendo!
(picha zote kwa uhisani wa internet)