Sunday, August 05, 2007

Matapeli wa Kishairi - Lyrical Crooks

Come listen to me
I made a discovery
I wanna share it with you
I have you know that is true

Multi-nationals are really criminals
all forms of gambling
there is no way you can win
open your eyes guys
its time you realize
that the rise in price
is to make more money
for those who has got plenty
and the trick of the trade
is to keep the hungry be listen empty

It’s the break of the day
its time you have to say
you have been sleeping all night
now its time for the light
come see lyrical crooks
who have learn their tricks by the books
so come disciples of god
who rule with an iron rod

Mtunzi: Bob Andy
Wimbo: Check it out
Album: Retrospective

Bob Andy katika wimbo huu anatutahadharisha na watu anaowaita “lyrical crooks” akimaanisha “matapeli wa kishairi” waliojifunza utapeli kwa kutumia vitabu, inawezekana ni kitabu cha Shakespeare au kile chetu cha abunuwasi au hivi vya kisasa na kidini. Watu wa aina hii wako wengi sana hapa kwetu na kibaya zaidi ni wale tunaowaamini sana, wanafanya maamuzi yakutuumiza halafu wanakuja na mashairi yao mazuri waliotumia muda mrefu kuyatunga na kuyakariri wakituhadaa tukubaliane na maamuzi yao kwamba yatatusaidia wakijua mwishowe ni matatizo kwetu na sio kwao.
Ingawa ni wimbo wa zamani kidogo lakini mtunzi alishaliona hili jinamizi la utandawazi kwa kupitia mtangulizi wake “Multi-nationals”au makampuni ya kimataifa! yenye utaifa! Sijui hawa watu huwa wanafikiria nini kwa dude hili, kuendeleza nchi? Kujiendeleza? Au kuingiza majina yao kwenye vitabu vya historia ( His-Story) kwamba waliwasaidia kukuza mitaji ya wale wanyehaki ya kuimiliki dunia? Nikiutafakari huu Utandawazi, huwa nashindwa kujielewa, hivi almasi na dhahabu nyingi zilizochimbwa Shinyanga na watu wasiokuwa wa-Tanzania, zikapelekwa Japan/Malaysia kuchongwa na Baadae kuuzwa kwenye soko la London na mapato yake kuhifadhiwa kwenye benki ya Australia zitanyanyua uchumi au pato la Tanzania kuliko ile kidogokidogo na itakayoendelea kuwepo kwa muda mrefu sana, iliyochimbwa Shinyanga, na wa-Tanzania, kisha kupigwa mnada Dar es salaam, bila kujali inapelekwa wapi, kisha mapato yake kuwekwa kwenye benki ya NMB! Lazima mmoja wetu atakuwa anakichaa! Na anacheza kamari, kama karata tatu, ambayo huna uwezo wa kushinda.
Wanaendelea na utapeli wao wa kishairi, wanapandisha bei kwa mashairi mengi yanayotuambia kuwa wanatujali! Huku wanachukua kidogo kwa wasionacho na kwaongezea wenye kingi sana! Na kuendelea kutubembeleza tuwasikilize wakijua tumeshakata tamaa.
Siku mpya itaanza tuu, tutaamka toka usingizi tuliolala siku nyingi sana, jua likituangazia tupate usemi wa kuwaambia tukiongozwa na mtume toka kwa mungu mwenye kuongoza kwa kutumia mkono wa chuma