Tarehe 17.01/2008 ilikuwa siku mbaya sana kwangu, baada ya kuwa na shaka ya siku tatu kuhusu hali ya mdogo wangu Majaheni T Newa nilipokea habari ya kusikitisha sana kuhusu kifo chake.Mazishi yalifanyika tarehe 19/01/2008.
Majonzi yaliyonikuta hapo sijui kama sio ndugu, jamaa na marafiki kunituliza yangenipeleka mahali ambapo hakuna ambaye angeamini.
Nashukuru wale walioshirikiana nami katika kipindi hicho kigumu na vilevile kuomba msamaha kwa wale ambao tukio hilo liliwagusa na tukashindwa kupatiana habari.
Pole sana Mloyi.Mwenyezi akupe nguvu katika wakati huu mgumu kwako na familia nzima.Poleni.
ReplyDeleteMloyi pole sana.Niko nawe katika kuomboleza...zemarcopolo
ReplyDeletePole sana kaka,ujazwe nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteKaka Mloyi pole sana ndugu yangu.Mapambano yanaendelea.
ReplyDeleteIRIE MAN.
Rasta hapa.
Poleni Mloyi.
ReplyDeletePoleni Mloyi.
ReplyDeletePole sana bwana mkubwa. Mungu akujalie nguvu uweze kuendelea na majukumu kama kawaida.
ReplyDeleteNimefarijika sana, sio kwa msiba tuu. bali kuona hata baada ya kupotea kwa muda mrefu sana bado mnapita kunitafuta. Changamoto kubwa sana kwangu kujiunga tena kundini.
ReplyDeleteTuendelee kuwa pamoja.
Aluta Continua.
Mkuu,
ReplyDeletePole sana. Namuomba Mwenyezi Mungu akurejeshee nguvu za mwili na imani. Amen.
F M Tungaraza.
Nice blog and article, thanks for sharing. However want to statement on few common issues, The website taste is great, the articles is in point of fact excellent
ReplyDeleteมาแล้วหนังออนไลน์สนุกๆ ดูหนัง Full HD ฟรี Alita: Battle Angel อลิตา แบทเทิล แองเจิ้ล (2019) ดูเมื่อไหร่ก็สนุก
ReplyDeletehttps://www.doonung1234.com/