Picha kwa hisani ya Charahani.
Nimepitia Blogu ya charahani leo nikakuta picha ya kuvutia sana.
Picha hii inaonyesha moja ya vijana wanajitahidi kujenga afya zetu kwa kutumia akili zao katika kilimo. inafurahisha sana kuona kwamba kuna vijana katika nchi hii wenye uwezo wa hali ya juu katika kilimo na kuzingatia wanaanzia bila mtaji wowote lakini wanafanikiwa kutunza bustani katika hali hii!
Hii inaonyesha jinsi tusivyohitaji wawekezaji toka nje katika sekta ya kilimo kama inavyosemwa na wachache kati yetu ikiwamo waheshimiwa wetu waliopo pale bungeni. Sijui hawa wanatoa wapi owoga walionao, nashangaa jinsi wasivyojiamini na kutodiriki kufanya uchunguzi wa kina ili watambue uwezo tulionao katika kilimo miongoni mwa vijana wa Tanzania. Naona hawa wachache bado hawajua faida ya kilimo kama biashara na kuainisha matatizo wanayopata wakulima wetu hata kushindwa kukiendeleza.
Ninasema kwa majigambo kuwa "wakulima" wetu wanafanya kazi kubwa sana na wanamafanikio mazuri sana ukiangalia mazingira wanayofanyia kazi, mitaji wanayoanza nayo na teknologia wanayotumia! kiasi wanachozalisha ni kikubwa sana na bado kuna uwezekano wa kuzalisha zaidi kama tunataka wafanye hivyo. Jana kwenye luninga wakulima wa mbinga walisema kwa mafunzo ya shamba darasa waliopata toka kwa mtaalamu wa kilimo katika wilaya yao wamefanikiwa kuzalisha kahawa nyingi kuliko walivyotegemea na walivyowahi kuzalisha.
Sijui kama hao wawekezaji katika kilimo watatoka kwa mungu, ambako hatuwezi kuhoji uwezo wao!, au watatoka bara jingine , ambao tukienda jifunza nao huwa tunaonyesha uwezo wa hali ya juu kuliko wao, ndio waje walete mapinduzi ya kilimo nchini mwetu! kichekesho kikubwa sana hiki.
Uwekezaji unaingia kwa kishindo katika kila sekta, sijui kama wananchi watapata nafasi huru ya kuwekeza katika sekta yeyote, tutaishia kushindana vita ya kushindwa na Bunge Ltd toka marekani wakati sisi tunanyimwa fursa ya kupata mitaji.
Sijui hizo sekta zinazopewa kipaumbele kama kusamehewa kodi kwa kipindi fulani, kutengewa maeneo maalumu na vituo maalumu vya kuwasaidia wanafaida gani kwetu kama kilimo kilivyo.
Sioni tutakachopoteza kama tunachopoteza kama hatutafanya chaguzi au tunavyofuga uzembe katika Tanesco, tukiweka pesa zetu kwenye kilimo ambacho ninakipa umuhimu wa hali ya juu kuliko sekta zote hapa nchini. Tunahitaji mapinduzi ya Kilimo kama tunataka maisha bora kwa kila mtanzania. Mapinduzi ya kilimo yatapatikana kwa njia zifuatazo;
-kuweka wananchi katika vikundi/ushirika wa kilimo
-kupatia hivi vikundi/ushirika uweza wa kukopa dhana za kisasa za kilimo
-kutoa mafunzo ya kilimo cha kisasa kwa vikundi/ushirika wa kilimo
-Kuhakikisha masoko yenye kutoa bei halali kwa mazao ya kilimo kama wafanyakazi wengine wanavyolipwa mishahara halali
-Kuhakikisha matendo ya ufisadi katika sekta ya kilimo yanakemewa kwa adhabu kali sana, hata kifo, kwa atakayepatikana na kosa la kuhujumu kilimo.
Hakuna Maisha bila kilimo.
Thursday, June 26, 2008
Subscribe to:
Posts (Atom)