Tuesday, January 10, 2006

Salaam ndugu...., habari za nyumbani? watoto?

Fikiria maisha yatakuwaje iwapo pale utokako nyumbani asubuhi kila uingiapo salamu zitafuata mlolongo huu.

Uingiapo kwenye Daladala unaanza kumsalimia mpiga debe ndugu habari za kuamka, nyumbani hawajambo, mama? watoto? halafu unahamia kwa konda, Habari gani? Vipi kazi leo? imeanza vizuri? mbona unaonyesho uchovu asubuhi hii yote? hukulala nini?. Naye konda anaanza kupita kwa kila mtu habari kaka/dada, Leo umechelewa kutoka? au mabasi ya shida leo? poleni sana, naomba nauli.

Mwendo unakuwa huu huu kwa kila unayekutana nae siku hiyo muuza chai, muuza machungwa,walinzi, makarani wa benki, watu wanaofanya promosheni maofisini na ndugu zao machinga, bila kusahau unaingia kwenye blogu zote unaweka salamu za asubuhi kwa kila moja.

Fikiria tena utatumia muda kiasi gani kutoa hizo salamu zote! utakuwa katika hali gani? utaweza kuendelea na kazi siku hiyo? Kazi ngapi zitasimama? foleni itakuwa kubwa kiasi gani?.

hivyo ndiya watu wanavyotaka iwe siku yao na wewe pia uwaige .

5 comments:

Christian Bwaya said...

Umezunguza jambo la maana sana. Umenipa changamoto!

FOSEWERD Initiatives said...

mambo ya blogu hayo....zamani nilikuwa ninashangaa wale watuma salamu wa RTD hadi wanachukua taji la taifa.....kumbe ukizoea inbakuwa sehemu ya maisha....tunashukuru kwa changamoto!

John Mwaipopo said...

Hii kali. lakini ndivyo tulivyo. Huku Marekani salamu sio lazima. Waweza kukaa katika nyumba uliyopanga kwa miaka hata 10 pasi na kumjua jirani yako nani, achilia mbali kumsalimia. Sisi tuliokulia katika nchi ambazo twaheshimiana na kusalimiana kila kukicha twapata taabu sana vile. Mtu mmoja ambaye amekaa hapa Marekani miaka 20 sasa anajuta kwa 'kupotoka' kwani at last he feels he doesn't fit in both worlds (kizungu kwa msisitizo tu). Bongo mgeni Marekani mgeni.

Ila ninachopata katika ujumbe wako ni kuwa too much nayo ni mbaya. Hakika utavuruga ratiba zako. Kila kitu kwa kiasi au vipi.

Reggy's said...

ndugu yangu hili suala linanipa sana shida niendapo Kijijini, maana ukijaribu kupita nyumba bila kusalimia wanasema mwana simon amerudi na kiburi, anajidai,... na mengine kedekede. naona hilo haliwezekanani mjini, lakini vijijini tulikozaliwa, bado ni muhimu labda kwa karne nyingi zijazo.

SaHaRa said...

Utamuduni huu uko sana vijijini. Wakati huko nje ndio kabisa hamna. Inaonyesha jinsi mbio za kutafuta maendeleo zinavyozidi na "ujirani na undugu" ndio unavyozidi kupungua kabisa.