Wednesday, March 29, 2006

Vibaraza vinaendelea.....

Vibaraza bado vinaendelea, kuna kipya cha Simba na Yanga lakini mwenyewe hasemi kama ni Simba au Yanga ,mimi naona kakaa kama Yanga vile,
Mtembelee hapa. Umuulize yeye ni simba au yanga, asipojibu shauri yake.
Mwandani sasa ameweka picha yake lakini sio mojakwamoja kama humjui huwezi kujua ni nani yule, lakini binti Simba anatuambia
huyu ni mwandani. Hilo afro bado lipo kama siku tulipoachana Tambaza Boys sekondari.
Yule mnakala maarufu wa mwananchi, Yahya cherehani na yeye pia ameingia kwenye blog,Naona sasa blog zinateka watu wote waume kwa wake wenye habari motomoto. Yeye
anashona kuliko cherehani ya mchina bila kutia umbeya na uwongo wa wanasiasa.
Ndesanjo naye kwenye nyumba yake mpya mambo bado ni moto sana.
Angalia kesho vibaraza vitakuwa vipi.

6 comments:

msangimdogo said...

Tunawakaribisha woooooote hawa wageni na wengine ambao watakuja siku zijazo

mwandani said...

Newa! tafadhali chunguza viungo ulivoweka, ikesha rekebisha kidogo.

nashukuru kwa kutupa jicho kila kona.

Jeff Msangi said...

Mloyi,
Ni faraja kujua kwamba bado upo nasi na sio kwamba labda JK ameshakupa kijinafasi pale Magogoni ukawa mwanzo wa kutupa kisogo.

MK said...

Samahani ingawa haya siyo maneno yanayo endana na kichwa cha habari lakini naomba nitoe tangazo langu kuhusu blog.

TANGAZO:

Baada ya uchunguzi wa hali ya juu nimegundua jawabu la kuondoa Blogger NavBar (Sehemu ya juu kabisa ya Blog yako inayo onesha search this blog).

Hii kutokana na ya kwamba watu wengi uwa wanachukizwa na jinsi hiyo NavBar ilipo.

Jawabu la hili swali unaweza kusoma kwa kubonyeza hapa

Kama ukipata tatizo au maswali zaidi naomba niandikie na nitakujibu asap.

Nashukuru,
©2006 MK

Imetengenezwa na kuletwa kwenu na ©2006 MK

Ndesanjo Macha said...

Rekebisha viungo Mloyi. Usiwe unaingia mitini namna hii.

John Mwaipopo said...

we unatafutwa hapa kibarazani. Bado kidogo tu tukaripoti kwa kamanda Chiko, sorry Tibasana, sorry Tibaigana.