Tarehe 17.01/2008 ilikuwa siku mbaya sana kwangu, baada ya kuwa na shaka ya siku tatu kuhusu hali ya mdogo wangu Majaheni T Newa nilipokea habari ya kusikitisha sana kuhusu kifo chake.Mazishi yalifanyika tarehe 19/01/2008.
Majonzi yaliyonikuta hapo sijui kama sio ndugu, jamaa na marafiki kunituliza yangenipeleka mahali ambapo hakuna ambaye angeamini.
Nashukuru wale walioshirikiana nami katika kipindi hicho kigumu na vilevile kuomba msamaha kwa wale ambao tukio hilo liliwagusa na tukashindwa kupatiana habari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
11 comments:
Pole sana Mloyi.Mwenyezi akupe nguvu katika wakati huu mgumu kwako na familia nzima.Poleni.
Mloyi pole sana.Niko nawe katika kuomboleza...zemarcopolo
Pole sana kaka,ujazwe nguvu katika kipindi hiki kigumu.
Kaka Mloyi pole sana ndugu yangu.Mapambano yanaendelea.
IRIE MAN.
Rasta hapa.
Poleni Mloyi.
Poleni Mloyi.
Pole sana bwana mkubwa. Mungu akujalie nguvu uweze kuendelea na majukumu kama kawaida.
Nimefarijika sana, sio kwa msiba tuu. bali kuona hata baada ya kupotea kwa muda mrefu sana bado mnapita kunitafuta. Changamoto kubwa sana kwangu kujiunga tena kundini.
Tuendelee kuwa pamoja.
Aluta Continua.
Mkuu,
Pole sana. Namuomba Mwenyezi Mungu akurejeshee nguvu za mwili na imani. Amen.
F M Tungaraza.
Nice blog and article, thanks for sharing. However want to statement on few common issues, The website taste is great, the articles is in point of fact excellent
มาแล้วหนังออนไลน์สนุกๆ ดูหนัง Full HD ฟรี Alita: Battle Angel อลิตา แบทเทิล แองเจิ้ล (2019) ดูเมื่อไหร่ก็สนุก
https://www.doonung1234.com/
Post a Comment