Wednesday, September 28, 2005

Karibuni

Kaa tuzumze,
tuongee mambo mazuri,
tuelewane kwa maongezi,
pesa za kidunia zisituingilie,
wahenga nawaalika,
kwa heri na busara,
shari ikae mbali,
hata wanyonge wajongee,
walio mbali watusikie,
wakaribu watuone,
wasiojua uzuri wa tausi,
hawajui thamani yake,
tupendao usikivu,
twajua busara zake,
kila mmoja anaijua,
hata kama hajaipata,
siwezi kuitaja,
msaada naomba,
niweze ipa jina,
na wote waipate....

5 comments:

mwandani said...

naam, twaib, tumeketi, hadithi njoo, utamu kolea!Karibu sana.

Ndesanjo Macha said...

Mloyi mwana wa Newa ingia ndani!

Indya Nkya said...

Karibu karibu mloyi
uandishi lazima ufanywe hata kwa gharama ya kuwakera watu, watakaokereka na wakereke, watakaofurahi na wafurahi, hatuandiki kumfurahisha yeyote wala kumhudhi yoyote, tunaandika tudhaniyo, kwamba ni mumuhimu kwa jamii.

NA WEKA MTAZAMO MAKINI said...

Varandani nimefika,vigoda vipo,ni mikeka, na kwa wale wenye utamaduni wa magharibi viti vipo pia
Safari ni ndefu karibu.

Dabra Makeda 8 said...

shukrani nimekaribia japo miguu haikunjiki, ila jamvini twaketi, gumzo likikolea hata kulala ni kheri ila hali tuu moto unakolea na kuni kuzichanja, yetu mashoka kiberiti shikilia kaka, wote ni wamoja. Bless.