Friday, February 24, 2006

Bado nipo..

Sio kama nimeondoka kimyakimya bado nipo ila mambo yaliingiliana kidogo ndiyo maana niko kimya. Wordpress imekuja kwa kishindo kama ilivyokuja Blogspot inatamanisha kuhamia kwenye hayo makazi mapya, bado ninafikiria kama yatakuwa mapya siku zote au ndiyo kilekile, kipya kinyemi na kuwa wa kileo hata kama hujafika leo!
Ndio ninapata matatizo kidogo kutumia blogspot, mpaka leo sijaweka picha yangu hapa,labda nimezoea "cut and Paste" iliyorahisi bila kuzungukia njia nyingine, lakini hapa tunapendana zaidi kupaacha sio rahisini kama kukubali kufa na kuwaacha uwapendao dunuani.
Mijadala inazidi kupanuka, kila kitu kinawekwa wazi hapa. Kuna kusanyiko la waandishi wa habari, wasomaji wa habari wanaopenda kugawia wenzao habari walizoziona kwenye sehemu mbalimbali, watu wa soga, watuma picha na wa udaku pia. Wanablogu wa kiswahili tumeungana kwa kiasi kikubwa, sote tunashirikiana na kujuana kwa majina ingawa hatujuani kwa sura, siwezi kusema kwamba hakuna wanablogu wa kiswahili walionje ya mtandao huu.
Blogu nyingi zimevuma hapa wakati kama hii yangu inatokea kwa nadra na bila viunganishi motomoto, ukitaka viunganishi motomoto unaweza kupitia makene, ndesanjo , Nambidza na kuzunguka kwenye blogu zote za kiswahili zilizo kwenye mtandao huu.
Ushirikiano na kutembeleana kati yetu tuuendeleze, tusiwaache wenzetu waliohapa maana wametueleza walipohamia hivyo bado tupo nao, tuwatembeleeni ili tuendelee kufaidika na mawazo na ufahamu wao.

7 comments:

boniphace said...

Afadhali nimejua huu mzima maana nilishaanza kuwaza kuwa nawe uliuliwa na polisi baada ya tukio lile lilioundiwa tume na JK. nATANIA HAPO. Lakini kweli tunafurahi kuwa unakuja kiasi hiki maana sisi nduguzo ambao hatujui sura yako tunapata tabu kila tupitapo nyumbani kwako hapa na kukuta mlango umefungwa. Haya karibu karibu usijali umeme wa mgawo una mwisho lakini vipi kuhusu mradi wa IPTL?

Reggy's said...

naona ulipowataka makene, ndesanjo na Nambiza, ulikosema viunganishi, blogu zao hazifunguki kupitia hapo. mie mzima

mloyi said...

Bado mzima na nipo.
Nimeweka viunganishi bubu, au vipofu! havikupeleki unakotaka, siku nyingine nitakuwa mwangalifu zaidi.
Mgao wa umeme unazidi kuwa mkali, sasa ni masaa 18 usiku mzima na sehemu ya mchana, najua Makene ameshasahau mambo haya lakini sisi huku bado tunayakumbatia! Sijui JK aige ya Ahmedinajan? Kama ana kiburi kidogo kuliko Mkapa, Kumbuka Mkapa alikataa kumwekea vikwazo Mugabe ingawa walitakiwa wafanye hivyo na Magharibi.
Mvua leo wingu ni kubwa kiasi imenyesha kidogo inabidi tuwahi mabasi, nadhani vipanya , vitufikishe nyumbani tujiandae na vua la usiku, kama mungu "ametuona".
Mengine hali ni ileile, nimesahau, Majambazi yametulia kidogo! sijui CUF wametii amri? kumbuka kauli ya Mahita. Sijui ataondoka rasmi lini.

mwandani said...

Motowaka haya! motowaka, vuuu, vuuu, vuuu!
puliza moto mwanangu, tunakuzengea hapa kibarazani kwako kila kukicha, bora umerudi utujulishe ya huko.

Ndesanjo Macha said...

Motowaka...king'ora kinalia. jamaa wa faya wanakuja kuzima moto!
Mambo?

mloyi said...

moto ukiwaka itakuwa balaa! ndesamjo vipi? mbona makazi yako mapya yamekuwa ubao wa matamgazo kama lile bango la jangwani!

John Mwaipopo said...

Wewe Mloy unatafutwa kibarazani hapa. Muda sio mrefu tutatuma ambyulensi na zima moto.