Wednesday, June 21, 2006
Afrika inathaminiwa vipi na ....
Wakati sisi tunawaza kwenda ughaibuni kutafuta maisha kuna wengine wanalilia kuja Afrika kutafuta maisha na kuishi, watu hawa wana sababu za msingi kuhusu uamuzi wao wa kuja kuishi na kuendesha maisha yao Afrika. Wimbi hilo la watu kuja kuishi afrika linaendelea hadi kwa waafrika wenzetu wanaoishi uhamishoni. Ingawa inakuwa vigumu kidogo kwao kuchagua mahali pa kuhamia lakini hawa wameshafanya uamuzi wao au wako njiani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
6 comments:
Ukiweza tunapulie kidogo taarifa hii kwa kuongelea watu kama akina Bupe, Robinson, Profesa Mkhululi na wengine waliohama Ughaibuni na kuhamia Tanzania.
Mimi siwezi kushangaa hata siku moja mtu mweusi akiamua kurudi Afrika. Hakuna mahali hata pamoja nilipokanyaga katika mabara yote ambako sijakuta Mtu mweusi hawezi kunyanyaswa kirahisi.Ni Afrika pekee mtu mweusi anakubalika. Afrika Pagumu lakini angalau hakuna ambayae anaweza kukufukuza kwa kukuambia ondoka barani kwetu
awalin ya yote nashukuru kwa kunitembelea na pia kuniakaribisha,naahidi kufanya hivyo mara kwa mara.
Nimevutiwa sana na habari ya Rita kutafuta ardhi Africa!hii inaonyesha ni kwa jinsi gani watu wanavyopenda kwao.hii pia inachangiwa na ubaguzi ulikithiri.Kwa mfano katika nchi za ulaya kuna kikundi kinajiita "Ku Clux Clan"Hawa hawapendi mgeni yeyote katika nchi zao.
Hata tukikataa Afrika bado ni eneo bikra kabisa kwa misingi ya hali ya hewa, dhana za watu maisha na kila kitu kwa hiyo sishangai hawa watu wanavyohamia na wengine kuwapo njiani.
Huku ni bara ambalo unaweza ukaja kuchukua vitu vya watu na wao wakakuangalia tu huku wakikupigia makofi na hata kukupongeza.
na wapo wengi tu ambao wanapaswa kurudi Africa.THE BLACKSTARLINER ije iwachukuwe hata kama ni kwa nguvu warudi nyumbani.
Napenda kumpa hongera mama Ritha Marley kwa uamuzi wake wa kuchagua Ghana, hii ni jinsi gani anavyothamini afrika kwa jinsi ilivyo si kwa jinsi ya maendeleo ya baadhi ya nchi, mana mpaka hivi sasa tumeshaona baadhi ya masupa star wanavyothamini baadhi ya nchi sababu ya maendeleo waliyopiga na kutozijali nchi masikini za afrika, huku wakidai wao asili yao ni afrika.Watu hawa utakuta wako bize kuja kula maraha kwenye miji kama Cape town huku wakizipa kisogo nchi zilizo nyuma kimaendeleo.
Wakaribishwe watu wote weusi wanaoithamini afrika kwa dhati na walaaniwe wote wanaodanganya na kuibeza(wanafki).
Mungu Ibariki Afrika
Post a Comment