Wednesday, October 12, 2005

Makosa na usahaulifu.

Barua niliyomwandikia ndugu yangu nkya, sijui kam inaukweli ndani yake au inaweza kutumika kuombea PHd kwenye fani ya siasa.
Ndugu Hilo ndilo kosa la ANC naona liko kama kosa la Nyerere, yeye hakuamini kama ujamaa unaweza kuanguka, ilikuwa ni dhambi kama kufikiria kuwa papa. Alijenga mashirika ya umma bila kuwapa umiliki wananchi hivyo ujamaa ulipoanguka na hayo mashirika yalishindwa kuendeshwa na wananchi, sasa wakipewa wazungu kuyaendesha tunapiga kelele bila kutafuta chanzo, angalia wachina naona mao alijuwa hiki kitu akaandaa watu wake ili kuwa tayari kumiliki uchumi iwapo ukomunisti ungeanguka ndiyo maana wachina hawanashida na mwekezaji toka ulaya.Kila mchina ana uwezo wa kutengeneza kitu ambacho sisi tunatumia dola nyingi kuviagiza. Sijui fani yako, lakini naona kama sio technolojia ya chuma uchumi wa ulaya usingekuwa hapo ilipo sasa, wameweza kutengeneza vyombo vya usafirishaji, mitambo na pia vifaa vya kilimo vilivyowapatia maendeleo ya haraka. Sijui kama wangengoja wa-kushi wawatengenezee hivyo vifaa wangekuwa wapi sasa?. Sina takwimu sahihi lakini naona kama technolojia ya chuma hapa Tanzania haithaminiwi ndio maana tunaingia karne ya 21 bado tunatumia jembe la mkono!. Marekani iliendelea kwa kuwafanya waafrika watumwa wao kwenye mashamba na migodi, hilo sisi hatuliwezi, lakini tunao ng'ombe wengi wenye nguvu kama nyati kwa nini tusiwatumie kukuza kilimo? Ukinichagua mimi nitaleta maendeleo bila wananchi kujifunga mkanda, ghafla mahitaji yatajaa madukani, na pesa mifukoni hawaongelei, ukweli ni havitakuwa vya waliowapigia kura! Angalia ikapa hapo, huna haja ya kuwasha gari kwenda kazini, unauhakika wa kupanda treni au kama ni mwoga 'Golden arrow' ipo. Nini maana yake 1. Unakuwa umetunza mazingira kwa kutotengeneza moshi mchafu kuliko ukoma. 2. Umepunguza mafuta ambayo serikali hutumia mamillioni ya pesa za kigeni kuyaagiza baada ya kuhudumia wakulima na sekta nyingine zenye umuhimu. 3. Badala ya kuendesha gari ukiwa peke yako na kuleta msongamano mjini, utaupunguza kwa kutumiausafiri wa jumuiya- ambao ni nafuu zaidi kwa gharama.
Hayo ndiyo maoni yangu. Mjadala uko wazi kuchangia.

5 comments:

Ndesanjo Macha said...

Mloyi, umesoma hoja za Fide kufuatia hoja yako kuwa sisi makabwela hatulipi kodi hivyo sio ajabu ndege ya sirikali ikibeba maiti za watoto wa matajiri?

Reggy's said...

nakushukuru kwa kazi nzuri. Umeanza vizuri na kazi hii ni ya kujituma haina malipo lakini inaridhisha moyo endapo utaiendeleza. Karibu sana. Viti mimi naviona, asiyeviona ana dhambi.

Rama Msangi said...

Kuna suala la dhamira, na hili nadhani ndio msingi mkubwa wa kila jambo duniani. Kila jambo linaanzishwa mwanzishaji akiwa na dhamira. Je, Nyerere alikuwa na dhamira ya kuona Watanzania tunaurejea utumwa kwa mlango wa nyuma?, hakika hapana ila kuna watu walimsaliti, na kwasababu hatuna hulka ya kunyoosheana vidole, ndio maana yanatukuta haya ya sasa

Ndesanjo Macha said...

Umeishia wapi????

FOSEWERD Initiatives said...

bwana mloyi,

labda nianze kuzungumzia hili la ANC. ndani ya ANC kuna muungano. bila muungano chama hakina nguvu. wanaiotwa triplate alliance. kuna COSATU - wafanyakazi, SACP chama cha kikomunisti na ANC yenyewe! hawa ndio wamempa mbeki nguvu na hutetemeka sana akisikia kuna ufa! naupenda sana utendaji wa ANC kwani unasikia haraka sana mambo yanayoyahusu makundi hayo! sio kama tanzania mseme msiseme chama cha nyerere kinapeta! Afrika kusini wamejifunza mengi toka kwetu hivyo raisi wake ana mrengo wa kulia! huyu anapigamia kuwa na uchumi dhabiti, bila kukosana na wawekezaji na wakati huo huo kunyanyua hali za maisha ya weusi kwa ule mpango wa Black Economic Empowernment! ninaweza kusema amefanikiwa japo mabadiliko hayaji kwa usiku mmoja, ni namba nzuri tu ya weusi ambao wanaendelea kunyanyuka siku hadi siku, Tatizo la waafrika wengine na hasa wale wenye fikra za ukombozi ili wawe wakubwa na sio ukombozi dhidi ya umasikini ndio wanatesa watu wao kila kukicha - mfano mugabe. kazi kubwa ambayo ndio unaiona ndani ya ANC ni kuweka uwiano kati ya uchumi na maendeleo. kwa sasa inaendelea vyema, japokuwa utakuta kuna kundi lenye mrengo wa kushoto (wasiotaka maridhiano)- la akina Zuma lilitaka kuwa na nguvu lakingi tunashukuru wameweza kubalance mambo!