Tuesday, May 23, 2006

Hawa wameumbwaje?

Burning Spear aliuliza hivi, ….Unakumbuka siku za utumwa? Babu zetu walivyochukuliwa kama vifaa vya kufanyia kazi. Wengine wengi mpaka leo wanahoji hivi utumwa ulikuwa halali? Maswali huwa hayaishii hapo tuu, mengine mengi hufuatia kama vile ukiwa Afrika na makazi ya waafrika kote duniani utasikia maneno haya …..Unajua hawa watu wa ulaya wanatunyonya sana! Ukiwa kwenye maeneo ya wazungu ukikutana na waafrika wengi wao watakwambia Unasikia bwana hapa tatizo kubwa ni kubaguliwa, tunachukuliwa sisi (waafrika) kama watu wa daraja la chini sana … Ukikuta maraisi wa Afrika kwenye mkutano wataongelea tofauti katika mgao wa biashara baina ya nchi za Afrika na za magharibi( Ulaya na Marekani) hawa hujadili njia madhubuti ya kuleta usawa na kuzinufaisha nchi za kiafrika katika biashara ya dunia.
Dunia nzima na sasa hata watoto wao wazungu sasa wameanza kuwasema baba, mama, babu na bibi zao kwa wanachowafanyia waafrika na wa-Asia kiasi cha kujitolea maisha yao kupambana na Dola zao. Lakini wengi wao hawatajibu au kufanya lolote kuhusu jambo hilo na wala hawatachukia maneno yako wala kuyafurahia.
Ukimsikiliza Tony Blair , Joji Kichaka na wengine wa aina hiyo watakubali machono mwako kwamba waafrika wanadhulumiwa na kuna haja ya kufanya mabadiliko ili kubadili mfumo uliopo sasa na kuahidi kutoa kipaumbale kwa jambo hilo.
Wataunda kamati za kushughulikia jambo hilo lakini matokeo yake yatakuwa labda hawataongelea tena matokeo ya kamati hiyo au ufumbuzi utakaotolewa utaleta matatizo na manung’uniko mengi zaidi!
Cha kushangaza ni uvumilivu wa wazungu kuhusu kauli zinazowakosoa na manung’uniko wanayopata kutokana na matendo wanayowafanyia watu wa asili nyingine tofauti na zao. Nashindwa kuelewa uumbwaji wao ulikuwa wa aina gani kwani sisi waafrika tukisemwa kidogo huwa tunajirekebisha na kufuata ushauri tuliopewa na “wenzetu”.

4 comments:

Indya Nkya said...

Mloyi ndugu yangu. Wao ni matajiri kwa vile sisi ni masikini. Ukweli ni kwamba ili maisha yetu yabadilike kuwa mazuri ni lazima yao yawe mabaya kiasi fulani. Hawako tayari kwa hilo. Hizo kamati za kina Be liar ni uhuni tuu. Ndio maana jina lake ni kuwa muongo!!

Anonymous said...

...please where can I buy a unicorn?

Anonymous said...

iAddeddazgReTllkq [url=http://bit.ly/oldnavycouponsbox]old navy coupons[/url] Veeippilsdlismp

obat vimax said...


Thanx for sharing ilike your book